Header Ads

Samia Suluhu: Mkilitumia vyema Soko hili litawasaidia kuepukana na Umaskini









Makamo wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh Sami Suluhu Hassani amewataka Wafanyabiasha wa wilaya ya Micheweni  kuwa wabunifu katika kuweza kuendana na soko la kiushindani.

Kauli hiyo ameitowa katika ufunguzi wa soko la konde wilayani hapa lilojegwa kupitia progiramu ya masoko ,uongezaji thamani na huduma ya kifedha kijijini{MIVARF}Zanzibar.

Makamo huyo amesema endapo wafanyabishara watalitumia vyema soko hilo litaweaza kuwasaidia kuondosha adha ya umbali mrefukutafuta huduma soka na baadala yake kutumia muda huo katika kazi nyengine za uzalishaji na maendeleo ya taifa.

Mh Samia ameongezakuwa kuwepo kwa soko la kisasa litapelekea kuongezeka kwa ajira ,kupitia kuongezeka kwa shughuli za kilimo na kipato cha mtu mmoja mmoja.

Kwaupande wake Waziri wa Kilimo,Mifugo,Maliasili na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid amewataka wananchi wa wilaya Micheweni kulitumia vyema ili kuweza kudumu kwa muda mrefu

No comments