Bodaboda Dodoma wanufaika na Kituo cha Mabasi Mkoani humo
KITUO cha mabasi yaendayo mikoani mjini Dodoma kimetoa
fursa za ajira kwa waendesha pikipiki –bodaboda- kutokana na mwingiliano wa watu
Wakizungumza na waandishi wa habari baadhi ya
waendesha bodaboda wamesema mwingiliano
wa watu katika mji wa Dodoma umesababisha
upatikanaji wa ajira kwao.
Pamoja na mafanikio hayo wamesema wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali kwa baadhi ya abiria kuwafanyia vitendo vya uhalifu
ikiwemo kuwanyang’anya pikipiki zao
Aidha wameiomba serikali kuwapatia elimu itakayo
wawezesha kujiunga na vikundi vitakavyowasaidia kutatua changamoto zao.
Kwaupande wa baadhi ya wanawake wanaojishughulisha
na biashara ndogondogo katika eneo hilo wamesema pamoja na kuwepo kwa biashara
ya bodaboda lakini biashara yao ya uuzaji wa zabibu imekuwa ngumu.
Post a Comment