Header Ads

Habari Zenye kuibua Changamoto za Mwanamke zahimizwa DODOMA


Waandishi wa Habari wakifuatilia Mafunzo ya Kuwajengea uwezo wa kuandaa taarifa na habari bora za vipindi vya Redio
Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika  habari zenye kuibua changamoto zinazowalenga wanawake katika jamii ili kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kudai haki zao.
Akiwasilisha mada kwenye mafunzo ya uandaaji vipindi na kuwajengea uwezo waandishi wa habari yanayoendelea mkoani Dodoma, Mwezeshaji kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO- BI ROSE MWALIMU amesema kuwa, bado wanawake nchini hawajapewa kipaumbele katika kupaza sauti zao jambo ambalo linawafanya kubaki nyuma kimaendeleo.
Bi Rose amesema kuwa ni asilimia 22 tu ya idadi ya wanawake ndio wanaoshirikishwa katika taarifa za habari ikilinganishwa na wanaume ambao ushiriki wao ni mkubwa .
Waandishi wa Habari wakifuatilia Mafunzo ya Kuwajengea uwezo wa kuandaa taarifa na habari bora za vipindi vya Redioyanayoendelea Mkoani DODOMA
(PICHA ZOTE NA GASPARY CHARLES.. MICHEWENI RADIO)

No comments