Header Ads

Ongezeni Mashirikiano kuboresha Ufanisi wa Shirika- M/kiti ZPC



Related image 
Bodi ya wakurugenzi ya shirika la bandari Zanzibar limewataka wateja wa shirika hilo Kisiwani Pemba kufanya kazi kwa juhudi na mashirikiano ili kuongeza ufanisi wenye kuleta faida kwa taifa na jamii kwa ujumla.
Hayo yamesema na Makamo Mwenyekiti wa bodi hiyo KHAMIS SALIM ALI huko ukumbi wa baraza la Mji Chake – chake katika kikao cha majumuisho ya ziara ya kutembelea na kuangalia shughuli za kiutendaji katika maeneo mbalimbali ya miundo mbinu ya shirika hilo.
Amesema mashirikiano ndio kitu pekee kitakacho lipeleka mbele shirika kwa kutoa huduma kiushindani na kuahidi kuyatafutia ufumbuzi yale yote yanayorejesha nyuma harakati za kiutendaji za shirika hilo.
Naye mjumbe wa bodi katika kikao hicho ALI MOH’D SHOKA amewataka wafanyakazi waongeze mapato na kuzuia mianya yote ya ukusanyaji wa mapato hayo.
Katika hatua nyingine baadhi ya wakuu wa vitengo vya bandari ya wete na wesha wamesikitishwa na kutokuwepo hati miliki katika maeneo ya usimamizi wa shughuli zao ambayo hivi sasa yameanza kuvamiwa na watu.

No comments