Wajasiriamali Kisiwani Pemba Wapata Elimu Mpya
WIZARA ya Kilimo ,
Maliasili ,Mifugo na Uvuvi, Pemba imewashauri wakulima na wajasiriamali
kuendeleza taaluma waliopatiwa juu ya isindikaji na usarifu wa mazao, kwa
wakulima wenzao, ili kuongeza ubora wa bidhaa wanazozizalisha.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Kiungo program za
ASSP/ASDP-L kutoka Wizara ya Kilimo, ASHA OMAR FAKIH, wakati wa uzinduzi wa
kituo cha usindikaji na usarifu wa mazao, huko Pujini, Mkoa wa kusini Pemba.
Aidha amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni
kuwawezesha wakulima kupata elimu ya kusarifu mazao yao katika ubora na utaalam
zaidi.
Kwa upande wake, muwezeshaji wa mafunzo ya
usindikaji na usarifu wa mazao, FATMA MOHAMMED MZEE, amesema kuwa uwepo wa
kituo hicho utasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza ubora wa uzalishaji na kupata
soko ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wao wakulima na wajasiriamali wameahidi
kuyatumia ipasavyo mafunzo hayo, ili waweze kujiongezea kipato kitokanacho na
mazao yao
Mafunzo ya usarifu wa mazao, pamoja na usindikaji
wa matunda na mboga mboga ni mafunzo ya siku nne yalioandaliwa na Program za
kuendeleza sekta ya kilimo na mifugo, ambayo yamewashirikisha zaidi wakulima waliopatiwa
taaluma ya uzalishaji, kati yao ishirini kutoka Mkoa wa kaskazini na ishirini
kutoka Mkoa wakusini Pemba.
Post a Comment