Rais wa Zimbabwe afanya majumuisho ya mafanikio yaliyopatikana tangu aingie madakarani
Rais
Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amefanya majumuisho kuhusu mafanikio
yaliyopatikana kwenye serikali yake katika siku mia moja za mwanzo tangu aingie
madarakani, na kuahidi kufanya mageuzi zaidi ili kuboresha uchumi wa nchi.
Rais
Mnangagwa aliyeingia madarakani tarehe 24 Novemba, amesema kazi zinazoikabili
serikali yake katika siku za baadaye zinahitaji juhudi za kila mtu, na
itachukua muda kabla ya matunda ya mageuzi kuonekana.
Rais
Mnangagwa amesema serikali ilipitisha bajeti yenye ufanisi ambayo inapunguza
matumizi yasiyo ya lazima, pia imeondoa sheria kadhaa za upendeleo, ili kuvutia
uwekezaji zaidi wa moja kwa moja kutoka nchi za nje.
Pia
amesema serikali yake imekuwa ikifanya juhudi za kujenga mahusiano ya kimataifa
na kuvutia uwekezaji, na hadi sasa imepata uwekezaji wa dola bilioni 3 za
kimarekani kutoka kwa makampuni makubwa duniani.
Post a Comment