Elimu Kilimo cha Kisasa kuwarahisishia wakulima wa Mwani Z'bar
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi na Bahari
Zanzibar Dk.Margareth Serapio Kyewalyanga amewataka Walikulima wa Zao la
mwani kutumia vyema mafunzo wanayopatiwa ya kilimo cha kisasa cha zao
hilo ili waweze kuzalisha mwani wenye ubora ambao utasaidia
kulipathamani zao hilo.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa semina ya
siku mmoja ya kilimo cha zao hilo katika maji makubwa amesema wakulima
watakapo yatumia vyema mafunzo hayo yatawasaidia kuzalisha zao la mwani
kwa wingi ambalo litawapatia kipato cha kujikimu na maisha.
Amesema ni suala zuri kuona wanawake
wanakuwa mbele katika kushiriki shughuli za maendeleo hivyo ni vyema
kuendelea kuthamini michango na elimu wanayopewa na tasisi mbalimbali
ili waondokane na utagemezi katika familia zao.
Aidha amesema wakati umefika kwa wakulima
hao kuachana na kilimo cha kizamani badala yake wajikite katika kilimo
cha kisasa ambacho kinawapunguzia hasara zinazojitokeza wakati wa
kuzalisha zao la mwani ikiwemo zao hilo kuuguwa maradhi.
‘’Kilimo hicho cha maji marefu
ni kizuri kwanza kinaepusha mwani kuuguwa maradhi kutokana na athari za
mabadiliko ya tabia nchi ambayo yasababisha mwani kuugua kutokana na
joto kali bahabari’’
Kwa upande wake amesema kwa sasa
wameanzisha mradi wa SEAPOWER ambao utawawezesha wakulima wa zao la
mwani kujua jinsi ya kuzalisha zao hilo katika maji ya kima kirefu ili
waweze kunufaika na kilimo chao.
Amesema katika kuhakikisha taaluma ya
kilimo hicho inawafikia wakulima kwa wakati Mradi huo pia umekusudia
kuendeleo kuhamasisha ukulima huo kwa kila kijiji ili weweze kuzalisha
mwani wa kutosha utakaoendana na mahitaji katika soko.
Amesema kilimo hicho cha kilimo cha mwani
katika maji marefu kutaengeza upatikanaji wa mwani kwa wingi hapa
Zanzibar pamoja na kuwawezesha wakul;ima hao kulima kilimo cha kisasa
kitakacho engeza thamani katika zao hilo.
Kwa upande wao wakulima wa zao hilo
wamesema licha ya kupewa mafunzo ya kilimo hicho lakini wanakabiliwa na
tatizo la kutojua kuogolea katika kima cha mqaji marefu ambapo zao hilo
linatakiwa kuoteshwa.
Wamesema watakapo letewa wataalamu wa
kuwafunza namna ya ya kukabiliana na mawimbi ya bahari kutawawezesha
kuendeleza kilimo hicho ambacho ndio tegemeo lao la kujikombo na
umaskini katika familia zao.
Wamesema kutoka na waume zao kuwa na
mwamko mkubwa wa kutoa ushirikiano katika kuwaruhusu kuendeleza kilimo
cha mwani watahakikisha wanatumia vyema mafunzo waliyoyata katika
kuengeza uzalishi pamoja na kujitolewa kuwafunza wakulima wengine ili
waweze kuimarisha uchumi.
Semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa
na Mradi wa SeaPower unaofadhiliwa na Serikali ya Australia na Swiden
imeshirikisha Wakulima wa zao la mwani kutoka sehemu mbali mbali ikiwemo
Kenya na Zanzibar pamoja na taasisi zinazosimamia masuala ya mwani na
Ununuzi.
Post a Comment