Kete 12 za Madawa zakamatwa MICHEWENI
KAMATI
ya ulinzi na usalama wilaya ya Micheweni ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo
SALAMA MBAROUK KHATIBU imefanikiwa kukamata kete 12 zinazosadikiwa kuwa ni dawa
za kulevya aina ya HEROINE katika eneo la kiuyu kipangani.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, ALIHAJI
HAJI KHAMIS HAJI amesema kuwa, kete hizo zimebainika baada ya kufanya upekuzi
kwa Kijana MWALIM IDDI MWALIMU 35, mkaazi wa Kinowe Jisu.
Kamanda
huyo amesema kuwa kijana huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi na Upelelezi
utakapokamilika atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Katika hatua nyingine kamanda HAJI amesema
kuwa katika Oparesheni hiyo wamefanikiwa kuwakamata vijana wanne waliokuwa
katika mazingira hatarishi
“jeshi
la polisi litawakama wale wote ambao wanajihusisha na vitendo vya kiuhalifu
ndani ya jamii “alisema kamanda haji.
Hata
hiyo mkuu wa wilaya ya Micheweni salama mbaruku khatibu amesema wamejipanga
kuhakikisha wameondoa kambi zote za madwa ya kulevya katika wilaya hiyo.
Salama
amesema kila maeneo ambayo yanatuhumiwa
kutumiwa madawa ya kulevya watakwenda kupekuwa ili kujuwa hali ilivyo.
“tutawatafuta
wahalifu wote kwa gharama yeyote ili kuwaondo wahalifu katika wilaya ya
Micheweni na mkoa wa kaskazni pemba kwa ujumla”alisema mkuu wa wilaya salama.
Oparesheni
hiyo imekuja kutokana na malalamishi ambayo wananchi waliyapeleka kwa mkuu wa
wilaya juu ya uwepo wa vikundi mbalimbali vya uhalifu katika maeneo yao.
Post a Comment