Migogoro ya Ardhi 'Kufuta Kazi Masheha' Zanzibar
MWENYEKITI
wa kamati ya baraza la Mapinduzi
inayoundwa na baadhi wa Mawaziri Mh. HAJI OMAR KHEIR amesema kuwa Serikali
haitakuwa na Dhamana ya kulinda kiongozi ambaye atabainika kuhusika na Migogoro
ya Ardhi.
Akizungumza
na viongozi wa majimbo, Madiwani, Masheha pamoja na viongozi wa kamati za
ulinzi na usalama Wilaya na Mkoa, amesema ni jukumu la viongozi hao kuhakikisha
wanasimamia na kudhibiti migogoro ya ardhi katika maeneo yao.
Amesema
zipo taarifa zinazowahusu viongozi na migogoro ya ardhi, na kwamba sheha
akibainika kuhusika, itakuwa ni kibali chake cha kufutwa kazi.
Kwa
upande wake mjumbe wa kamati hiyo Dk. SIRA UBWA MWAMBOYA amesema Serikali
imebaini kuwepo matumizi mabaya ya mashamba ya eka, hivyo inakusudia kuya[potia
upya ili kuyatambua mashamba hayo.
Mapema
mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mh OMAR KHAMIS OTHIMAN amesema kwa
Kushirikiana na Viongozi wa Shehia, Madiwani pamoja na kamati za ulinzi na
usalama wamefanikiwa kudhibiti migogoro ya ardhi katika Mkoa huo.
Post a Comment