Unaijua Haki yako ya Urithi?.
Jamii imetakiwa kuwa na
muamko katika kutafuta hati za umiliki wa
mali mapema ili kuwapa urahisi watoto kutoingia katika
migogoro ya urithi baada ya wazazi wao kufariki.
Wakizungumza na Micheweni FM
baadhi ya wanawake wa mkoa wa kusini walioshindwa kupata haki zao
baada ya wazazi wao kufariki dunia kutokana na kukosa
hati za umiliki tangu kwa uhai wa wazazi wao.
Wamesema kutokana na kukosa
haki zao mapema imeweza kuleta migogoro kwa familia na kupelekea
kushindwa kupata ushahidi wa kutosha juu ya idadi halisi ya
mali zao.
Aidha wamesema licha ya
jitihada wanazozichukua katika kutafuta haki zao lakini
wanashindwa kutokana jamaa zao kutowapa ushirikiano ya kutosha hivyo
wametoa wito kwa wazazi nchini kuzingatia umuhimu wa kutafuta hati
za kumiliki mali mapema kwa lengo la kuwaondoshea usumbufu watoto wao hapo
baadae.
Post a Comment