'Wazanzibar Tutembelee Maeneo ya Historia Kujifunza'
Wananchi wametakiwa kuwa na
mwamko wa kutembelea sehemu za kihistoria ili kujua historia ya nchi yao pamoja
na kujifunza utamaduni uliopo Zanzibar.
Akizungumza na Micheweni FM Ofisini kwake
Kisonge Mjini Unguja, Msimamizi wa Makumbusho katika mnara wa kumbukumbu
Kisonge Maneno Ibrahim khamis amesema baadhi ya wananchi hususan vijana
wamekuwa na muamko mdogo wakujitokeza katika maeneo ya kihistoria na kupelekea
kutojua historia ya nchi.
Amesema Zanzibar ni sehemu
ambayo ina utajiri mkubwa wa kihistoria hivyo ni vyema
wananchi kutembelea maeneo hayo ili kujifunza watanufaika na vitu vingi ikiwemo
kujua matukio mbalimbali yaliyofanyika Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi.
Aidha amesema kujua historia
ya Nchi itawawezesha vijana kutambua mila na desturi za wazazi wao na
kuachana na mila za Nchi za kigeni ambazo zinaharibu utamaduni wa mzanzibar
hususani kwa vizazi vijavyo.
Hata hivyo amesema ukuwaji wa
uchumi unachangiwa na sehemu za kihistoria kutokana na wageni kutoka nchi mbali
mbali kuja kujifunza Historia ya Zanzibar hivyo ni vyema kwa wananchi
kuimarisha mashirikiano katika kujifunza ili kuchangia pato la taifa letu.
Post a Comment