'Viongozi Halmashauri, Baraza la Mji Toeni mrejesho wa Mapato na Matumizi'
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Hifadhi wa Msitu wa Asili Ngezi
(NGENARECO) Hassan Suleiman Khamis amesema utafiti uliofanywa na Jumuiya hiyo
umebaini kuwa baadhi ya wananchi hawaelewi bajeti za Halmashauri na Mabaraza ya
Miji .
Akizungumza na wadau wakati wa uzinduzi wa Mradi wa
Kuhamasisha Uwajibikaji Zanzibar (PAZA) kwenye ukumbi wa mikutano wa Benjamini
Mkapa , amesema wananchi wanahaki ya kufuatilia na kuhoji mapato na matumizi
hasa wakati huu ambapo Serikali iko kwenye mfumo wa Ugatuzi wa Madaraka .
''Serikali imeshusha madaraka kwa wananchi , hivyo viongozi wa
Halmashauri na Mabaraza ya Miji wanapaswa kutoa mrejesho kwa wananchi pamoja na
kuweka wazi bajeti zao '' alisisitiza.
Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mohammed Nassor Salim amesema
mradi huo umelenga kuhamasisha sualala uwajibikaji kwa viongozi wa Serikali
pamoja na wananchi kushiriki kikamilifu kulinda miundombinu katika maeneo yao.
Amesema imebainika kwamba bado wananchi hawana taaluma na uelewa
wa kuilinda miundombinu , na kwamba Mradi huo utahakikisha kwamba kila mmoja
anakuwa mlinzi wa miundombinu hiyo.
'' Bado jamii inaonekana kuwa na dhana potofu ya kuona kwamba
miundombinu iliyowekwa ,jukumu lakuilinda nila serikali pekee , jambo ambalo
linapelekea jamii kushindwa kuchukuliwa hatua wakati wanaaposhughudia
uharibifu '' alieleza.
Mapema akizindua mradi huo kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa
Baraza la Mji Wete , Salma Khamis Juma amewataka wadau hao kuhakikisha
wanaihamasisha jamii kushiriki kazi za maendeleo .
Aidha amesisitiza haja lwa viongozi kusimamia vyema majukumu yao
ya kazi , na kuwashirikisha wananchi wakati wa kupanga na kuchagua miradi ya
kutekeleza .
''Ni vyema kila kiongozi kusimamia
kwa uwadilifu shughuli zake za kazi , kwa kuongeza uwajibikaji , ambapo hii
itasaidia kuwafanya wananchi kujua kazi zinazzotekelezwa na serikali kupitia
Halmashauri na Mabaraza ya Miji '' alisisitiza.
Mradi huo wa uhamasishaji uwajibikaji
Zanzibar unatekelezwa katika wilaya sita , ambapo kwa Pemba utatekelezwa katika
Wilaya ya Micheweni, Wete na Chake Chake .
Post a Comment