Header Ads

Fahamu Siri ya LAKI MOJA ilivyo wafanya 'Tupate Sote' Kuwa kikundi Tajiri Wilayani CHAKE CHAKE Kisiwani Pemba


Image result for ujasiriamaliWANAWAKE wa kijiji cha Mvungwa shehia ya Mbuzini wilaya ya Chakechake kisiwani Pemba, “tupate sote” walioanza na mtaji wa shilingi 104,000 kwa njia ya hisa mwaka 2016, sasa wanamiliki mtaji wa zaidi ya shilingi milioni 11 baada ya kuibua miradi mipya nane.

Miongoni mwa miradi hiyo ambayo inawaendeshea maisha yao na kusau ajira ya serikali, ni pamoja na kilimo cha mkusanyiko wa mboga, ushoni wa mikoba ya kisasa inayotumia punje, kili, vipochi, achari ya mbirimbi.

Miradi mengine ilioibuliwa na kikundi cha “Tupate sote” ni sabuni ya maji, mshuka ya kisasa, kilimo cha sun flower, ujenzi wa jengo kwa ajili ya kuweka mashine ya kukamulia na kusafishia mafuta ya sun flower , ambapo miradi hiyo inathamani ya zaidi shilingi milioni 11 hadi sasa.

Katibu wa kikundi hicho Meiye Hamad Juma, alisema kumbe walikuwa na fursa kwa muda mrefu za kuukimbia umaskini, ingawa wao wenyewe pamoja na wanaharakati, walichelewa kuwaamsha.

Alisema, baada ya wanaharakati kutoka Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA, ofisi ya Zanzibar na taasisi ya Milele Foundations kushirikiana kuwapa taaluma na vifaa vya kuanzisha uwekaji wa fedha na kukopa, hapo ndio iliokuwa mwanzo wao wa kupata manufaa.

Aidha Katibu huyo alisema, wakati wa uwekaji wa hisa ukiendelea na kilimo chao cha migomba, wakiendelea kukitunza, ghafla walipewa elimu ya ushonaji wa mikoba ya kisasa inayotumia ukindu, na shilingi 95,000 zikatumika kwa kugharamia mikoba mitano.

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Semeni Soud Seif, alisema mikoba hiyo iliongeza pato lao, maana baada ya kuiuza walijipatia shilingi 250,000 ambazo ziliwawezesha kubuni kilimo cha sun flower, na kujipatia lita 60 za mafuta safi, walizoziuza shilingi 240,000.

No comments