'Madereva Pemba acheni Kupandisha Nauli kiholela'
Madereva Wilaya
ya Wete wanaochukua Abiria wa Melini Mkoani wete wametakiwa kuacha
tabia ya kupandisha bei kiholela na badala yake wasubiri bei ambazo
zitatangazwa na serikali kisheria.
Hayo yamelezwa na katibu Tawala
Wilaya ya Wete Mkufu Faki Ali wakati akizungumza na Madereva hao
hapo Ofisini kwake Wete.
Amesema kumekua na malalamiko mengi
kutoka kwa abiria juu ya nauli walizoziweka Mkoani na Wete jambo ambalo
sio utaratibu uliowekwa kisheria.
Aidha amesema wanaopaswa kupandisha
bei za abiria ni wizara husika inayoshughulikia masuala ya usafirishaji
ndio wenye mamlaka ya kutangaza bei mpya na sio jambo jema kukaa
madereva kuweka bei mpya kinyume na sheria .
Nao Madereva hao wamesema
changamoto kubwa inayopelekea kufanya hivyo ni kutokana na upandishwaji
wa kodi mara mara ambapo kunawapelekea kuweka bei hiyo.
Kwa upande wake Afisa usafirishaji
Pemba Khamis Ali ameeleza kuwa mwenye mamlaka ya kutangaza bei mpya
ni Mh Waziri pekee na kuataka madereva hao kukaa na taasisi husika ili kutatua
changamoto zao.
Hata hivyo amesema licha ya
kupandishwa kwa bei ya mafuta lakini ni vyema kuendelea na utaratibu ule ule
uliopo wa nauli kwa wananchi na waache kuwasumbua.
Post a Comment