Header Ads

Mwakilishi Micheweni Akabidhi Mifuko 100 ya Saruji Kukamilisha Ujenzi Ukumbi Skuli ya Kiuyu Mbuyuni


Mifuko 100 ya Saruji iliyokabidhiwa na mwakilishi wa jimbo hilo, Mhe. Shamata Shaame Khamis, kwa uongozi wa Sikuli ya Kiuyu Mbuyuni, Wilaya ya Micheweni.
JUMLA ya mifuko 100 ya Saruji, imekabidhiwa katika uongozi wa Sikuli ya Kiuyu Mbuyuni, wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba ili kukamilisha ujenzi wa ukumbi wa kufanyia mitihani katika skuli hiyo.

Akikabidhi saruji hiyo, mwakilishi wa jimbo hilo, Mhe. Shamata Shaame Khamis, amesema kuwa ununuzi wa saruji hizo umetokana na mfuko wa mwakilishi wa jimbo.
Mwakilishi wa jimbo la Micheweni, Mhe. Shamata Shaame Khamis, akimkabidhi Mifuko ya Saruji, Kaimu mkuu wa skuli ya Kiuyu, Mwalim Mkasha Shaame Mbwana wakati wa zoezi hilo.
Mhe. Shamata amesema kuwa kukamilika kwa upatikanaji wa mifuko hiyo ni miongoni mwa hatua za utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi –CCM- waliyoiahidi kwa wananchi.

“Hizi ni miongoni mwa ahadi za ilani ya  CCM ambazo Rais wetu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,         Mhe. Dok. Ali Mohamed Shein anaendelea kuzitekeleza katika Nyanja mbalimbali,” alisema Khamis.

Kaimu Mkuu wa Skuli ya Kiuyu Mbuyuni, Mwalim Mkasha Shaame Mbwana, baada ya kupokea Mifuko hiyo.


Aidha kwa upande wake Diwani wa Wadi ya Kiuyu Maziwang’ombe, Ali Mkasha Mpemba, amempongeza mwakilishi wa jimbo hilo kwa juhudi zake za kuendelea kusimamia ipasavyo mahitaji ya wananchi katika jimbo lake.

“Juhudi hizi anazoendelea kuzifanya mwakilishi wetu, niwazi kwamba anatakiwa kupongezwa na kuungwa mkono kwani anajitahidi kukamilisha mahitaji ya wananchi katika jimbo letu,” alisema Mpemba.

Nae Kaimu mkuu wa skuli ya Kiuyu, Mwalim Mkasha Shaame Mbwana, ambae amekabidhiwa saruji hiyo, ameshukuru uamuzi wa mwakilishi  huyo kuamua kutenga kiasi cha fedha kwa ajiri ya kuwezesha ujenze wa ukumbi huo.

“ tunawaomba viongozi wengine kuiga kama huyu kwani anafanya kazi ya jamii na si yamtu mmoja mmoja na kuifanya jamii kuweza kumuamini”alisema mkasha.

Amesema hatua hiyo imekuja kufuatia kuwepo kwa uongozi madhubuti unaoongozwa na rais Dok. Ali Mohamed Shein unaozingatia usawa na utawala bora.
Mwakilishi wa jimbo hilo, Mhe. Shamata Shaame Khamis, (kulia) akipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa viongozi katika Skuli hiyo mara baada ya kukabidhi Mifuko ya Saruji.
Mwakilishi wa jimbo hilo, Mhe. Shamata Shaame Khamis, (Kushoto), akisikiliza maelekezo kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Skuli hiyo, Mwalim Mkasha Shaame Mbwana mara baada ya makabidhiano.

(PICHA ZOTE NA GASPARY CHARLES- MICHEWENI RADIO)

No comments