TRA: Mapato yanayokusanywa Zanzibar yanapelekwa Hazina Kuu
MAMLAKA ya Mapato
Tanzania (TRA) Ofisi ya Zanzibar imesema mapato yanayokusanywa
na Mamlaka hiyo kwa upande wa Zanzibar , zinabaki kwenye mfuko Mkuu wa hazina wa Serikali ya Mapinduzi
na zinatumika kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi
wa Zanzibar.
Afisa wa Elimu kwa
mlipa Kodi wa Mamlaka hiyo Zanzibar Abdalla Seif Abdalla
amesema tofauti inavyodaiwa na baadhi ya watu kwamba fedha hizo hupelekwa Tanzania Bara na kwa wananchi wa
Zanzibar hawanufaiki na mapato yao .
Akizungumza na
waandishi wa habari kutoka vyombo vya mbalia mbali vya habari , kwenye ukumbi wa Baraza la Mji Chake Chake
Abdalla amewataka
waandishi wa habari kutumia vyema vyombo
vyao vya habari kuwaelimisha wananchi jinsi fedha hizo zinavyotumika .
“ Fedha
zinazokusanywa na TRA kwa upande wa Zanzibar kuingizwa kwenye mfuko mkuu wa hazina Zanzibar na zinatumika katika
shughuli za
maendeleo kwa wananchi wa Zanzibar na sio
vyenginevyo ”alifahamisha.
Naye Afisa
Mdhamini Mamlaka ya Mapato (TRA) Pemba Habib Sultan amewataka waandishi wa habari kushirikiana na
watendaji wa Mamlaka kutoa
elimu kwa wananchi hususani wafanyabiashara kutambua umuhimu wa kulipa kodi .
Amesema kulipa kodi ni jambo la lazima kwa anayestahili , hivyo ni jukumu la waandishi wa habari kuvitumia vyombo vyao vya habari kuifikisha elimu ya kulipa kodi kwa wananchi , ili kila nayestahili aweze kushiriki katika kuchangia uchumi wa nchi .
Akitoa neno la
shukrani , Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari Pemba (PPC) Said Mohammed ameahidi kuwa waandishi wa
habari
wataendelea kushirikiana na TRA kuhamasisha
wananchi kulipa kodi .
Aidha amesema
kupitia taarifa na vipindi ambavyo vitaandaliwa pia vitatumika kuwafichua wafanyabiashara wanaokwepa
kulipa kodi ili
waweze kuchukuliwa sheria stahiki .
“Nikuahidi kwamba
sisi waandishi wa habari tutauendeleza ushirikiano uliopo kwa kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kulipa
kodi pamoja na
kuwafichua wafanyabiashara wanaokwepa kulipa
kodi ”alisisitiza.
Akifunga kikao hicho
Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake Suleiman Said Zahran
amemwataka waandishi wa habari kuongeza juhudi za kuwaelimisha wananchi ili waweze kujitokeza kulipa kodi jambo
ambalo litasaidia kukua uchumi wa taifa .
Hata hivyo amesema pamoja na changamoto mbali mbali zinazowakabili , ikiwemo ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi wanapaswa kuwa wazalendo wa taifa lao kwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuangalia maslahi ya nchi .
Post a Comment