Naibu Waziri SMZ Aonya Watakao 'Fisadi' fedha za miradi ya serikali
NAIBU Waziri Wizara ya Nchi Ofisi ya
Rais Tawala Za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za Serikali Mh Shamata
Shaame Khamis amewataka maafisa na chuo cha Mafunzo Pemba kufanya
kazi kwa uaminifu sambamba na kutoa taarifa kwa yeyote atakaeonyesha viashiria
vya kufanya ubadhirifu wa fedha za miradi ya serikali.
Akizungumza na
Maafisa wa Chuo cha Mafunzo huko Tungamaa ikiwa ni
muendelezo wa ziara zake za kukagua ujenzi wa nyumba za kuishi pamoja na ofisi
za maafisa na wapiganaji wa kikosi hicho , mhe Shamata amesema ni
vyema kuonesha uaminifu wa hali ya juu katika kusimamia na kuiendeleza miradi
hiyo .
Nae kamishna wa vyuo vya mafunzo
Zanzibar ALI ABDALA ALI amempongeza rais wa Zanzibar DR ALI MOHD SHEIN kwa
kuwapatia fedha za ujenzi wa nyumba hizo sambamba na kuwashukuru mafundi wenye
dhamana ya ujenzi kwa hatua waliyofikia .
Mkurugenzi Mipango , Sera na Utafiti
Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum
za Serikali Abdalla Issa Mgongo amesema kiwango cha fedha
kilichotumika katika ujenzi huo zinaendana na hali ya hatua za majengo zinazoendelea.
Post a Comment