SIRI MATOKEO MABAYA KWA WANAFUNZI YABAINIKA, DC MICHEWENI ATOA AGIZO ZITO KWA WALIMU, WAZAZI
UTORO, Malezi
hafifu, na Ufuatiliaji mdogo wa wazazi, vimetajwa kuwa chanzo kinachopelekea
Wanafunzi wengi kufeli katika Mitihani yao mbalimbali ya kitaifa Wilaya ya
Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba.
Hayo yamebainishwa
katika kikao cha wazazi, kamati ya Skuli, Walimu pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo Bi
Salama Mbarouk Khatib, katika Ukumbi wa Skuli ya Karume Msingi iliyopo Shumba
ya Mjini wilayani hapo.
Wakichangia katika
kikao hicho cha kutathimini sababu za wanafunzi kuendelea kufanya vibaya katika
mitihani ya Taifa, wazazi hao wamesema zipo sababu mbalimbali ambazo hupelekea
matokeo mabaya kwa wanafunzi.
Asha Nassor
Abdallah, amebainisha na kusema kwamba wazazi hasa wa kiume, wamekosa
ufuatiliaji kwa watoto wao na kupelekea watoto kuwa watoro.
Asha Nassor Abdallah, Mzazi akichangia katika kikao hicho |
Mwalimu mkuu wa Skuli ya Karume, Nassor Omar
Bakar, alisema licha ya juhudi zinachukuliwa na walimu kufundisha lakini
upungufu wa Walimu pia nalo no tatizo katika ufaulu wa Wanafunzi.
Mwalimu mkuu wa Skuli ya Karume, Nassor Omar Bakar, akifungua kikao hicho |
Akijibu baadhi ya
maoni ya wazazi, Mkuu wa Wilaya hiyo Salama Mbarouk Khatib, aliitaka kamati ya
skuli kukutana pamoja na wazazi ili kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya
wanafunzi.
“Niwaagize kamati
ya Skuli, tafteni siku mkae pamoja na wazazi ili kutafta msitakabali wa
maendeleo ya wanafunzi kwani hatuwezi kufumbia macho watoto wetu kuendelea kufelim,”
alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, Salama Mbarouk Khatib, (katikati) akiandika maoni ya wazazi wakati wa kikao hicho ambapo alikuwa mgeni rasmi. |
Aidha pia alishauri
wazazi na walimu kukubalina pamoja ili kuwawezesha watoto kupatiwa fursa ya
kuwa wanasomeshwa masomo ya Ziada.
Sikuli ya Karume
Msingi iliyopo Shumba Mjini Wilaya ya Micheweni ni Miongoni mwa Skuli katika Wilaya
hiyo zilizofanya vibaya katika Mitihani ya Darasa la Nne na Sita kwa mwaka
2017.
Post a Comment