'SMZ Ajirini Wataalamu wa Lungha za Alama'
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshauriwa kuimarisha Miundombinu pamoja na kuajiri
wataalamu wa lugha za Alama katika Vituo vya Afya ili kuwawezesha watu wenye
mahitaji maalumu (Walemavu) kunufaika na huduma za matibabu.
Akizungumza
wakati wa kuwasilisha ripoti ya watu wenye ulemavu kwa Mkoa wa
Kusini katika muendelezo wa Mkutano wa utekelezaji wa mradi wa
kushajihisha Uwajibikaji Zanzibar PAZA katika Ukumbi wa Ofisi za TAMWA Tunguu.
Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Watu ulemavu Mkoa wa Kusini Unguja Yunus Kassimu
Khatibu amesema watu wenye ulemavu wanapata tabu wakati wanapohitaji
huduma za afya kutokana na kushindwa kuwasiliana na Baadhi ya Madaktari juu ya
matatizo yanayowakabili.
Amesema
licha ya kuandaliwa mazingira Bora kwa Baadhi ya Majengo ya Umma lakini
bado katika Vituo vya Afya vya mjini na vijiji upatikanaji wa huduma
za afya umekuwa si rafiki kwao.
’’serikali ituangalie sana sisi walemavu
tunapata tabu hususan wenye ulemavu wa kusikia baadhi ya madaktari hawatufahamu
tunapotaka kuwasiliana nao bora tuekewe wataalamu wa lugha za alama kwenye
vituo vya afya ili watusaidie katika mawasiliano ’’Alisema Yunus.
Akizungumzia
suala la Miundombinu rafiki katika Majengo ya Umma ikiwemo skuli amesema Bado
suala hilo ni Tatizo kwao jambo ambalo linawakosesha Fursa za
Elimu katika Baadhi ya skuli za Msingi na secondary pamoja
na Vyuo vya Elimu ya juu.
Amesema
licha ya watu wenye ulemavu kuwa na muitikio mkubwa wa kupata elimu lakini
jitihada zao zinaishia njiani kutoka na kukabiliwa na matatizo mbali mbali
wakati wanapohitaji elimu hiyo ikiwemo miundombinu isio rafiki pamoja na kukusa
Nyenzo za kufundishiwa jambo ambalo linawakosesha fursa za kufaulu.
Mwenyekiti
huyo Alisema “
miundombinu rafiki katika vituo vya afya pamoja na maeneo ya maskulini yamekuwa
yakiwakwamisha watu wenye ulemavu katika jamii na kupelekea kushindwa kupata
huduma bora ambazo wanazipata watu wengine licha ya kuwa na
sisi tunauwezo wa kuzipata’’
Akitowa
ufafanuzi juu ya suala la Miundo mbinu ya vituo vya afya Vilivyomo katika Mkoa
wa Kusini Daktari Zamana wa Wilaya ya kati Tatu Ali Amour amesema tatizo la
miundo mbinu linatokanana na vituo vingi vilivyopo katika mkoa huyo vimejengwa
kwa ramani za kizamani ambazo hazijazingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji
maalum (WALEMAVU).
Amesema
katika kukabiliana na tatizo hilo Serikali ya inaendelea na Azma yake ya kutoa
huduma bora kwa wananchi ikiwemo kujenga majengo ya kisasa yenye kuendana na
mahitaji ya kila mwananchi.
Mkutano
wa umeandaliwa na Chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA kwa kushirikiana
na Jumuia ya Waandishi wa habari za maendeleo Zanzibar (WAHAMAZA),Jumuia ya
Kuhifadhi maliasili za asili Pemba NGERANECO chini ya Taasisi zisizokuwa
za kiserikali ZANSAZP ili wananchi wajuwe haki zao na watendaji wajuwe wajibu
wao katika kuwasaidia wananchi.
Post a Comment