Idadi ya vifo kutokana na mlipuko mjini Kabul, Afghanistan yafikia 57

Wizara ya
afya ya umma ya Afghanistan imesema mlipuko uliotokea jana karibu na kituo cha
kuandikisha wapiga kura mjini Kabul, umesababisha vifo vya watu 57 na wengine
119 kujeruhiwa.
Kwa mujibu
wa wizara hiyo, wengi wa waliouawa ni raia wa kawaida, wakiwemo wanawake 21 na
watoto watano, na kundi la Islamic State limetangaza kuwajibika na shambulizi
hilo.
Imefahamika
kuwa uchaguzi wa bunge nchini Afghanistan utafanyika Oktoba 20 mwaka huu, na
kazi ya kuandikisha wapiga kura imeanza Aprili 14 kote nchini humo.
Post a Comment