Mawaziri wa mambo ya nje wa China na India wakutana Beijing
Waziri wa mambo ya nje wa China Bw
Wang Yi jana alikutana na mwenzake wa India Bibi Sushma Swaraj mjini Beijing.
Bw Wang Yi amesema kwamba rais Xi
Jinping wa China atafanya mkutano usio rasmi na waziri mkuu wa India Bw
Narendra Modi tarehe 27 na 28 mwezi huu mjini Wuhan mkoani Hubei, China.
Nchi zote mbili zinatakiwa kufanya
maandalizi ili kufanikisha mkutano huo, kuzidisha ushirikiano kati ya pande
mbili, na kutoa mchango katika kuhimiza maendeleo na amani ya kikanda na ya
dunia nzima.
Kwa upande wake Bibi Sushma Swaraj
amesema India inapenda kushirikiana na China kuhimiza urafiki na kuinua kiwango
cha kuaminiana, na kuimarisha uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo
mbili.
chanzo: chinaswahili
Post a Comment