Header Ads

Kuelekea Mei Mosi, DC Micheweni atoa neno kwa Wafanyakazi



WATUMISHI wilaya ya Micheweni wametakiwa kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kufuata taratibu za utumishi wa umma ili kuwahudumia wananchi kama inavyotakiwa.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya hiyo, Salama Mbarouk Khatib, baada ya kushiriki zoezi la usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni.

Salama amesema kuwa iwapo wafanyakazi watafanya kazi zao kwa kuzingatia taratibu za utumishi wa umma itawajengea imani kwa wananchi wanao wahudumia.

“imefika wakati wafnayakazi tunahitaji kubadilika, tujitahidi sana kutekeleza kufanya kazi kwa kuzingatia maadili kwani kwa kufanya hivyo itatuongezea imani kwa wananchi wetu” alisema Salama.

Aidha katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amewapongeza wafanya kazi wa Hospitali hiyo kwa kuendelea kutoa huduma bora kjwa wananchi.
“Nichukue pia nafasi hii kuwapongeza wafanyakazi wote wa hospitali hii kwani mumekuwa mkijitahidi kutekeleza majukumu yenu kama inavyotakiwa” alisema.

Kwa upande wake Dakitari dhamana katika hospitali hiyo Dakitari Rashid Daudi Mkasha, amemshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa uamuzi wake wa kushiriki zoezi la usafi katika Hospitali hiyo ikiwa ni moja ya Shamra shamra za kuelekea kilele cha siku ya Wafanyakazi Duniani.

“Tukushukuru sana Mkuu wa Wilaya pamoja na Wafanyakazi wote mliojitokeza katika zoezi hili, kwani ni wazi kuwa mmefana kazi kubwa na sisi tutaendeleza pale tulipoishia,” alisema Dok. Rashid.

Zoezi hilo la kufanya usafi ni miongoni mwa shamrashamra za kuelekea maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani ambapo kitaifa yanatarajia kufanyika Mkoa wa Kaskazini Pemba.

MATUKIO KATIKA PICHA 
Baadhi ya Watumishi waliojitokeza katika zoezi hilo wakiendelea na Usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni
  
PICHA ZOTE NA GASPARY CHARLES- MICHEWENI REDIO

No comments