Mvua yawakosesha Makazi Watu Saba Wilaya ya WETE
MVUA zinazoendelea
kunyesha zimesababisha watu saba wa familia ya Said Mohammed Salim
wa Gando Wilaya ya Wete kukosa sehemu za
kuishi kufuatia nyumba yao ya kuishi kubomoka baada
ya kuangukiwa na muwembe .
Tukio hilo limelazimu Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Wete
ikiongozwana Mwenyekiti wa Kamati hiyo Abeid Juma Ali kufika katika eneo
la tukio kwa lengo la kuifariji familia hiyo .
Akizungumza katika eneo la tukio Mwenyekiti wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama Wilaya ya Wete ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya
hiyo Abeid Juma Ali amewataka wananchi kuchukua tahadhari ya
kuiondoa miti ambayo imeshaanza kuoza kwa kufuata sheria ya ukataji
miti hasa katika kipindi hichi cha mvua za masika.
Aidha mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa serikali kupitia kamati
ya maafa ya wilaya itaangalia uwezekano wa kuisaidia faamilia hiyo hasa katika
kipindi hichi na kuwataka kuwa wastahamilivu .
Nae mwathirika wa tukio hilo Said Mohammed Salim
ameishukuru serikali ya wilaya kwa kuwa karibu na wananchi wake jambo ambalo
linawawezesha pia kufika katika eneo la tukio kwa wakati.
Post a Comment