Miamba sita hatarini kushuka Ligi Kuu Pemba
WAKATI Ligi Kuu ya Zanzibar
kanda ya Pemba ikielekea ukingoni, timu sita zipo kwenye hatari ya kushuka
daraja msimu ujao.
Miamba hiyo ni pamoja na
Okapi, Chuo Basra, Younger Islander, Dogomoro, FSC na Kizimbani.
Baadhi ya timu hizo tayari
zimebakiwa na michezo mitatu na nyengine miwili.
Hata hivyo, ligi hiyo imefikia patamu kwa timu zilizoko katika nafasi ya kuwemo kwenye nne bora ambazo hatimaye zitacheza hatua ya nane bora ya Ligi Kuu ya Zanzibar.
Vigogo hivyo ni Mwenge, Opec,
Rock, Jamhuri, Shaba, Chipukizi, New Star na Wawi.
Mwenge ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikijikusanyia pointi 47,ikifuatiwa na Opec yenye pointi 43,Hard Rock pointi 40 na Jamhuri yenye pointi 38.
Katika mchezo uliopigwa
uwanja wa Gombani juzi huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha, Kizimbani iliibuka
na ushindi wa magoli 7-1 dhidi ya Okapi.
Mchezo huo ulishuhudiwa na
mashabiki wachache uwanjani hapo huku baadhi yao wakipiga kelele wakidai
kulikuwa na upangaji wa matokeo.
Magoli ya Kizimbani
yalifungwa na Khatib Hassan (dk.ya 11 na 63), Abdalla Hamad (dk.ya 57,69 na
84), Mohamed Seif (dk.ya 78) na Ali Othaman Ali (dk.ya 66).
Okapi walipata bao la kufutia
machozi kupitia kwa Suleiman Amour kwenye dakika 18.
Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wa Okapi walionekana wakali kwa wenzao kutokana na kuruhusu magoli mengi kama hayo.
Kufuatia hali hiyo, wachezaji
wawili wa safu ya ulinzi ya Okapi, Khatib Hassan na Hamad Seif waliamua kucheza
nafasi za mbele kutokana na mashabiki kuwashtukia kucheza chini ya kiwango.
Post a Comment