Header Ads

VYOMBO VYA HABARI PEMBA VYAPEWA JUKUMU LA KUELIMISHA JAMII ULIPAJI WA KODI

WAANDISHI wa Habari Kisiwani Pemba wameshauriwa  kuielimisha jamii juu ya suala  la ulipaji wa kodi,kwa lengo la  kuisaidia Serikali kupata mapato kwa maendeleo ya Nchi .

Wito huo umetolewa na Afisa Mdhamini Mamlaka ya Mapato Pemba Habibu Saleh Sultani watakati alipokuwa akizungumza katika Mafunzo na Waandhishi wa habari wa vyombo mbalimbali Kisiwani Pemba.

 Amesema ni Vyema Wananchi kufahamu kuwa kodi ambazo wanatozwa zinatumiwa na Serikali katika huduma  zote  za kijamii  ikiwa lengo ni kuwasaidia wanachi wake.

Nae Mwakilishi wa Jimbo la Chake chake  Mh Suleiman Said Sarahani amesema  Mwandishi wa habari anamchango mkubwa katika kuielimisha jamii ,hivyo ni vyema wawe mstari wa mbele katika kutoa elimu ya ukusanyaji wa kodi .

Akiwasilisha mada kwa wandishi wa habari hao Afisa Elimu kutoka Mamlaka ya Mapato  Abdalla Seif Abdalla amesema Kulipa kodi ni alama ya uzalendo ,kwani lengo laSerikali  ni kukusanya zaid mapato  ili kutoa huduma  za kijamii na maendeleo.

Akitoa neno  la Shukrani Mwenyekiti wa  Jumuia ya Wandishi wa Habari Pemba Said Mohamed amesema elimu waliyoipata wataitumia katika kuwaelimisha jamii huku wakifichua wanaokwepa kulipa kodi  ili kuisaidia Serikali kutokosa mapato yake.

No comments