Msemaji wa serikali ya Uganda asema kitendo cha kuipaka matope China hakitafanikiwa
Msemaji wa Serikali ya Uganda
Bw. Ofwono Opondo ametoa makala kwenye gazeti kubwa la nchi hiyo the New Vision
akisema, kitendo cha kuipaka matope China hakitafanikiwa.
Kwenye makala hiyo Bw. Opondo
amesema rais Donald Trump wa Marekani amekuwa akiongea mara nyingi kwenye
ukurasa wake wa Twitter kwamba mgogoro wa kibiashara utaleta faida, na Marekani
itashinda kwenye mgogoro huo kwa urahisi. Lakini hajui kuwa muundo wa dunia
umebadilika kwa kiasi kikubwa.
Amesema ingawa Marekani
inadumisha hadhi yake kuwa nchi yenye nguvu kubwa zaidi duniani, lakini tabia
yake ya ujeuri haikubaliki.
Pia amesema jaribio lake la
kuipaka matope China halitakuwa na mafanikio, kwa sababu ustawi wa China na
ushiriki wake kwenye mambo ya kimataifa vimeleta utulivu wa kisiasa, usalama wa
kijamii na maendeleo ya kiuchumi kwa nchi zote duniani zikiwemo nchi za Afrika.
Pia anaona ni jambo zuri kwa Serikali ya China kutangaza kuchukua hatua za
kujibu hatua ya Marekani kutoza ushuru wa forodha dhidi ya bidhaa za China.
Post a Comment