Header Ads

MTIBWA SUGAR v SIMBA SC HESABU GANI?


Image result for MTIBWA SUGARKipute kimoja cha mchezo wa ligi kuu bara kinapigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambapo Mtibwa watakuwa wenyeji kuikaribisha Simba.

Timu zote zinakutana zikiwa na kumbukumbu ya kushinda michezo yake ya ligi iliyopita ambapo Mtibwa waliilaza 3-0 Singida United na Simba wakiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Njombe Mji FC.

Mtibwa wametamba kuelekea mchezo huo kuwa hawana hofu na Simba na dozi waliyowapa Singida United wataihamishia Uwanja wa Jamhuri leo.

Kupitia Msemaji wa Mtibwa, Thobias Kifaru, tayari ameshaweka tambo zake akisema hawana hofu na Mnyama kutokana na kasi waliyokuja nayo.

Mtibwa imeshinda mechi zake mbili mfululizo zilizopita ikiwemo dhidi ya Azam FC kwenye FA na Singida United katika ligi.

Mchezo huo utaanza saa 10 kamili jioni ya leo.

No comments