Waziri Mohamed: Saratani Mlango wa Kizazi inazuilika
WAZIRI
wa Afya, Hamad Rashid Mohamed, amesema, Ugonjwa wa Saratani ya mlango wa kizazi
unazuilika kwa chanjo, hivyo amewataka wasichana kupata chanjo hiyo mara
itakapoanza kutolewa hivi karibuni.
Hayo
ameyasema wakati alipofungua mkutano wa uhamasishaji kwa wakuu wa mikoa na
wilaya juu ya uanzishwaji wa chanjo mpya ya kinga dhidi ya saratani ya mlango
wa kizazi jana.
Amesema,
saratani ya mlango wa kizazi ndio inayoongoza kwa kuathiri akinamama wengi
nchini Tanzania ikiwemo Zanzibar ambapo akinamama 51 kati ya 100,000 moja
wanaathirika na ugonjwa huo.
Aidha,
amesema, akinamama 38 kati ya 100,000 hufariki kila mwaka kwa saratani hiyo na
inakadiriwa kuwa wastani wa wanawake 466,000 wanagundulika kuwa na saratani ya
mlango wa kizazi kila mwaka na wengi wanaoathirika wanatokea nchi
zinazoendelea.
Hivyo,
amewataka wananchi kuitumia fursa hiyo ambapo amesema chanjo hiyo
ni salama na imethibitishwa na Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) na itatumika
kwa wasichana wenye umri wa miaka 9 hadi 14.
Post a Comment