AU kuisaidia DRC kudhibiti mlipuko mpya wa Ebola
KITUO cha kudhibiti na kuzuia
magonjwa cha Afrika (Afrika CDC) kimeanzisha operesheni ya dharura ya kuunga
mkono juhudi za Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC katika kupambana na
mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola nchini humo.
Serikali ya DRC imetangaza
kuibuka tena kwa Ebola Jumanne wiki hii, baada ya sampuli mbili kuthibitishwa
kuwa na virusi vya ugonjwa huo EVD mkoani Equateur nchini humo.
CDC Afrika itatuma timu ya
kudhibiti milipuko ya magonjwa ambayo itajumuisha wataalamu wenye uzoefu wa
kukabiliana na Ebola ilipolipuka mwaka 2014 katika Afrika Magharibi na mwaka
2017 nchini DRC.
Post a Comment