Waziri: Ni Marufuku Daktari Kumuuzia Mgonjwa Damu
WAZIRI wa Afya Mhe. Hamad Rashid Mohd
amesema ni dhambi kubwa kwa daktari kumuuzia mgonjwa damu kwani damu
inatolewa bure kwa mgonjwa nayehitaji kuongezewa damu .
Mhe Hamad ameyasema hayo wakati
akizindua bonanza la uchangiaji wa damu kwa mkoa wa kaskazini pemba
katika viwanja vya Jamhuri wilaya ya wete.
Amesema hatakuwa tayari kuona wananchi
wanauziwa damu na kwamba atakaye bainika atamchukulia hatua kwa mujibu wa
sheria.
Naye mwananchi Hamad Mbwana Shaame
amewataka wananchi kujitokeza kufanya uchunguzi wa afya zao ili waweze
kujifahamu na kuchukua hatua za kujilinda iwapo watagundulika kuwa wana maradhi
.
Post a Comment