'Malezi ya Pamoja yanahitajika Kudhibiti Mporomoko wa Maadili katika Jamii'
BAADHI ya wazee katika Wilaya ya Wete
wamezungumzia suala la kuporomoka kwa maadili ndani ya jamii na kusema chanzo
ni kukosekana kwa malezi ya pamoja .
Wakizungumza na mwandishi wa habari
hizi baadhi ya wazee akiwemo Suleiman ali haji mkazi wa Kizimbani amesema suala
la malezi ya pamoja na linahitaji kurejeshwa ili kudhibiti mporomoko wa maadili
.
Naye Bi Asha Hamad aAi amewataka
wananchi kushirikiana katika malezi ya watoto kwa kila mzazi kuwa na uwezo wa
kumchukulia hatua mtoto wa mwenzake anapofanya kosa.
Afisa ustawi wa Jamii Wilaya ya Wete Bi Nafhat Suleiman Yahya ameishauri jamii kurejea katika mafundisho ya Dini pamoja
na wanaume kujua majukumu yako.
Post a Comment