Elimu mbadala kuendelea kutoa mafunzo kwa Vijana Zanzibar
MKURUGENZI wa Elimu Mbadala na watu
wazima Zanzibar Mashavu Ahmada Fakih amesema kwamba Idara yake itaendelea
kutoa mafunzo ya fani ya taaluma ili kuwajengea uwezo vijana walioshindwa
kuendelea na masomo na watu wazima kujiajiri au kuajiriwa.
Amesema lengo la Idara hiyo ni
kuwajengea uwezo wawezeshaji katika vituo mbalimbali ,kutumia mbinu
shirikishi kuwawezesha wanafunzi kupata ufaulu kuendana na
mabadiliko ya kidunia ya sayansi na tecknologia.
Mashavu amesema hayo katika kituo
cha Elimu Mbadala Wingwi Wilaya ya Micheweni alipokua akifungua mafunzo ya siku
tisa kwa wawezeshaji wa vituo vya elimu mbadala na fani ikiwa ni mfululizo wa
mafunzo endelevu kwa watendaji wake.
‘’Idara imeandaa mafunzo haya kwa ajili
ya kuwajenga uwezo walimu wanaosomesha madarasa ya elimu mbadala na watu wazima
ili waweze kupata mbinu za kuwafundisha na kuongeza ufaulu ’’alieleza.
Amesema saikolojia yakufundisha watu
wazima inataka busara ,upole, upendo na utulivu ,hivyo amewataka
wawezeshajai hao kutumia lugha nzuri kwa kutambua shida zao na kuishi nao
kirafiki ili kuona mafunzo hayo yanawatoa katika kufanyakazi kwa mazoea
na wanatumia elimu wanayoipata .
Aidha Mashavu amefahamisha kwamba Idara
imeanzishwa mitaala ya somo la kiingereza kwa wanakisoma , ili kuwajengea
mazingira mazuri ya kujiajiri kupitia sekta ya utalii .
Mratibu wa Elimu Mbadala na Watu Wazimu
Pemba Hija Hamad Issa amewasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kutumia
maarifa baada ya mafunzo kuwawezesha kutumia vitabu na mbinu mpya kwa faida yao
na taifa.
Amesema kuwa mafunzo hayo yataleta
mabadiliko katika utendaji wao wa kazi , ambapo wanatakiwa kutumia
mbinu ambazo zitawafanya wanafunzi kupenda kuhudhuria masomo yao .
Naye mwalimu wa somo ya Saikolojia Haji
Juma amesema kuundisha mtu mzima yataka moyo wa ujasiri na upendo ili kuweza
kufanikisha lengo lililokusudiwa .
Hivyo amewataka washiriki wa mafunzo
hayo kuhakikisha wanakuwa karibu na wanafunzi kwa kujenga nao urafiki na
kuwasaidia wanapokuwa na shida .
Post a Comment