Mlemavu wa Akili aliyepewa Ujauzito Wilayani Wete, Mama mzazi alaani Unyama aliofanyiwa Mwanae
MAMA mwenye mtoto ambae ana ulemavu wa akili mkaazi
wa shehia ya Shengejuu Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, amesema kudhalilishwa kwa mwanawe
na kupewa ujauzito ni mitihani kwake na kamwe hatokwenda kushitaki
popote.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwa mama huyo, alisema kuwa mwanawe huyo
anawatoto wawili ambao amewapata kwa njia ya kudhalilishwa, ingawa hajavifikia
vyombo vya sheria kuripoti.
Alisema
anaona bora kumshitakia Mungu kwa kitendo anachofanyiwa mwanawe,
kutokana na kuwa anapoulizwa hawatambui wanaomfanyia ukatili huo, hivyo ni
vigumu kwenda kuripoti kwenye vyombo husika.
“Kwa
kweli ni mitihani kwa sababu kila siku ukimuuliza alikuwa anataja mtu mwengine,
kwa hiyo hatujui tumkamate nani, hivyo tumeamua kukaa tu na kumuachia Mungu”,
alisema mama huyo.
Mama
huyo, aliiomba Serikali kuwasaidia huduma zote ikiwemo chakula, matibabu na
malazi ili kuendesha maisha yao, kwani hali yao ni masikini huku watu
wakiwaongezea mzigo katika familia.
“Nashindwa
hata kuwahudumia watoto vizuri huduma zinazostahiki, kwani mwanangu ni mlemavu
wa akili na sasa ana watoto wawili wanaohitaji kushughulikiwa”, alisema mama
huyo.
Nae
dada wa msichana huyo, alisema kuwa hali ya watoto hao hairidhishi
kiafya kutokana kukosa chakula chenye lishe bora na kwa wakati, hali ambayo
inasababisha kudhoofika kimwili pamoja na kuvamiwa na maradhi ya kila aina.
“Kwa
kweli ni mitihani lakini anavyofanyiwa mdogo wangu ni ukatili mkubwa, familia
yetu ni masikini na bado watu wanatuongezea mzigo,” alisema dada huyo.
Nae
msichana huyo mwenye ulemavu wa akili, alisema kuwa aliyembaka na kumpa
ujauzito mara ya pili anamjua ni mkaazi wa Mgogoni Wilaya ya Wete Mkoa wa
Kaskazini, ambae alikwenda shengejuu kutembea kwa jamaa zao na ndipo
aliposubiri wazazi wake wamekwenda shamba na kwenda kumbaka nyumbani kwao.
“Alikuja
nyumbani watu hawapo akanibaka, nilipokuwa na mimba nilimwambia lakini
alikimbia na kwenda Mgogoni hadi leo sijamuona na wala haniletei huduma”,
alisema.
“Mwanangu
hapati chakula mpaka watu warudi shamba wapike, tunakula usiku, maana sina pesa
ya kumnunulia chakula chakumpikia, hivyo hukaa na njaa muda mrefu na maziwa
hayamshibishi tena”, alisema.
Msaidizi
mratibu wa shehia hiyo, Maryam Said Ali, alisema wakati wa tukio
hilo kutokea walikwenda kuwashauri wazazi wafike vyombo vya sheria kuripoti,
ingawa walishindwa kwa madai kuwa hamtaji mmoja anapoulizwa mtoto wao.
“Mara
zote tulizokwenda alikuwa anamtaja huyo huyo, kinachonishangaza wazazi wanasema
eti anataja wengi hawajui wakamate wapi, lakini ninavyoona wanakataa muhali
maana huyo mwanamme ni katika familia yao na ndio maana hawakufika kwenye
vyombo vya sheria kuripoti”, alisema Mratibu.
Nae
,Sheha wa shehia hiyo, Omar Faki Kombo, alisema kuwa wazazi wa msichana huyo
wamekuwa hawasemi mara zote anazowafuata kutaka taarifa, jambo ambalo
limepelekea kesi hiyo kutoshughulikiwa.
“Wazazi
hawako tayari kusema hili, pia mtoto mwenyewe hana mtu mmoja anaemtaja
nimelibaini hilo, hivyo tunaomba vyombo vya sheria pamoja na wadau mbali mbali
kushirikiana kwa pamoja, ili kuona msichana huyu anapata haki zake za msingi na
huduma”, alisema sheha huyo.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, Haji Khamis Haji, alisema
hajapokea taarifa hiyo na kuwataka wananchi wasivunjike moyo katika
kuripoti kesi hilo, ili kuweza kupata haki zao za msingi.
Post a Comment