Dawa za Kulevya Bado Kitendawili Pemba, mwingine akamtwa tena na kinachodaiwa kuwa Bangi
MKAAZI
wa singida Edward bundalla (50) anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoa wa
Kaskazini Pemba baada ya kukamatwa akiwa na majani makavu yanayosadikiwa kuwa
ni bangi nyongo 748.
Akithibitisha
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ,kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba ,
kamishina msaidizi Haji Khamis Haji amesema bundala amekamatwa na askaari wa
jeshi la polisi katika bandari ya wete muda mfupi baada ya kushuka kwenye
chombo akitokea Tanga kuja Pemba .
Amesema kuwa
mtuhumiwa huyo bado anaendelea kushikiliwa na jeshi la Polisi na uchunguzi
ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili .
“Mtuhumiwa
tunaendelea kushikilia na kumfanyia mahojiano na upelelezi ukikamilika
atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili,” alifahamisha.
Aidha
kamanda Haji amesema kwa hatua ya kwanza Jeshi la Polisi linajiandaa kuyapeleka
majani hayo kwa mkemia mkuu wa Serikali ili yakafanyiwe uchunguzi wa kisayansi
.
Akizungumzia
suala la uwepo wa Bandari bubu nyingi mkoani hapo , Kamanda Haji amewataka
wananchi wanaoishi karibu na zmaeneo hayo kushirikiana na jeshi la polisi kwa
kutoa taarifa wanapobaini kuna vitendo vinavyoashiria uhalifu .
Kamanda wa
Polisi ameeleza kwamba jeshi la Polisi litaendelea na operesheni ya kamata
wasambaji, wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya na kwamba watatekeleza
operesheni hiyo bila ya kumuonea mtu.
Post a Comment