Uhamiaji Zanzibar yawaongezea Elimu Wadau wake
IDARA ya Uhamiaji Tanzania kwa upande wa Zanzibar
imetoa Semina Elikezi kwa wadau wa huduma za uhamiaji Kisiwani Pemba ikiwa ni
katika kuhahikisha taarifa za wageni na wahamiaji nchini zinapatikana kutoka
kwa wadau hao.
Akifungua Semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi
wa Baraza la Mji Chake Chake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman
Abdalla amesema wadau wa uhamiaji wana mchango mkubwa katika kuona nchi
inaepukana na wahamiaji haramu.
Mapema akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Afisa uhamiaji
Mkoa wa Kusini Pemba Abdi Bulushi Juma ameseme lengo la semina hiyo ni
kuimarisha biashara na utalii nchini.
Kwa upande wake Khamis Breki ambaye ni mtembeza
watalii amesema kuna vikwazo vikijitokeza wakati wakitembeza wageni kutoka
katika mamlaka za nchi , huku Mlenge Moh`d kutoka jeshi la polisi akitaka kujua
mchango wa diaspora walioko katika nchi mbali mbali kwa taifa.
Semina hiyo elikezi iliwashirikisha madereva wa
tax, watembeza watalii, wahudumu na wenye mahoteli, askari wa jeshi la
polisi, kamisheni ya utalii na wadau wengine mbali mbali wanaohusiana na
masuala ya uhamiaji.
Post a Comment