Pombe Haramu, Dawa za Kulevya zinavyoteketeza Vijana Wilaya ya Micheweni, Serikali yaamua kuingilia kati
SERIKALI ya
Mkoa wa Kaskazini Pemba imesema vita dhidi ya dawa za kulevya haitakoma licha
ya baadhi ya wananchi kutoridhishwa na juhudi zinazochukuliwa katika
kukabiliana na matendo hayo.
Mkuu wa Mkoa
huo Omar Khamis Othman ameyaeleza hayo baada ya kushiriki zoezi la kuteketeza
madumu 39 ya pombe haramu aina ya Gongo katika shehia ya Kifundi Wilaya ya
Micheweni.
Amesema
msako wa kuwasaka wanaofanya biashara hiyo ni endelevu ambapo wananchi
wanatakiwa kutoa taarifa kwa viongozi wakiona kuwa viashiria vya biashara
hiyo.
Madumu hayo
yamekamatwa wakati wa opresheni ya kupaambana na madawa ya kulevya
inayosimamiwa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib.
Amesema kazi
zinazofaanywa na vikosi vya ulinzi Wilaya ya Micheweni kwa kushirikiana na
Polisi Jamii, zinapaswa kuungwa mkono na kima mmoja kwani zina lengo la
kudhibiti matendo maovu ikiwemo wizi wa mzao na mifugo.
‘Natoa
pongezi kwa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na polisi jamii kwa kufanikisha
kukamata madumu haya, kama yasingekamatwa vijana wengi wangeathirika,
iendeleeni na kazi hii na S erikali ya Mkoa iko pamoja nanyi” alisema.
Naye kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Abeid Juma Ali amesema serikali itapambana na mtu
yeyote na wa aina yeyote na wakati wowote ikiwa atabinika kujihusisha na
vitendo viovu ikiwemo uuzaji wa pombe haramu na dawa za ulevya.
Ameeleza
kuwa Serikali itapambana na mtu yeyote na wa aina yeyote ambaye tutambaini kuwa
na anachangia kuharibu afya za wananchi wetu .
“Mtu yote
ambaye atabainika kuharibu afya za wananchi tutapambana naye, wapeni salamu,tutahakikisha
tunawatafuta popote na mahala popote walipo ’’alieleza.
Kwa upande
wake Fakih Yussuf akizuzngumza kwa niaba ya Jeshi la Polisi Mkoa huo amewataka
wananchi kudumisha ushirikiano na jeshi la polisi hasa katika kipindi hichi cha
kuelekea mfungo wa mwezi wa ramadhan kwa kutoa taarifa sahihi zinazohusu
matukio au viashiria vya kufanyika uhalifu.
Fakih
amesema bila ya wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi, itakuwa ni vigumu
kuweza kudhibiti matendo maovu , na kuwapongeza Polisi waliofanikisha
kukamatwa kwa pombe hiyo kabla haijaingia sokoni na kuathiri vijana wengi
ambao ni nguvu kazi ya taifa.
Hata hivyo
Hamad Bakar kiongozi wa Polisi Jamii kijini cha Kipangani Shehia ya Kifundi ,
ameiomba Serikali ya Mkoa kuwapatia vitendea kazi ikiwemo viatu kwa ajili ya
kutumia wanapokuwa katika operesheni .
Amesema
polisi jamii weengi wamevinjika moyo kutokana na kukosa kipato kama walivyodhania,
na waliobaki watahakikisha wanafanya kazi hiyo kwa moyo na juhudi zao zote,
wakitekeleza kazi ya kujitolea.
Zoezi la
kuteketeza pombe hiyo haramu limefanyika katika kituo cha Polisi Matangatuani
Shehia ya Kifundi na kuhudhuriwa pia na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya
ya Micheweni.
Post a Comment