Kenya inataka hatua thabiti kulinda misitu ambayo inapungua
MKE wa Rais wa Kenya Bi.
Margaret Kenyatta ametoa wito kuchukuliwa hatua kwa haraka na thabiti ili
kurejesha na kulinda misitu ambayo inazidi kupungua nchini humo.
Bi. Margaret amesema
inahitajika azma ya pamoja na uthubutu wa wakenya wote ili kurudisha misitu
iliyofutika kufuatia shughuli za kibinadamu na uharibifu uliotokana na
mabadiliko ya hali ya hewa.
Akizungumza hayo kwenye msitu
wa Kibiku katika kaunti ya Kajiado, alisema suala hilo halihitaji kusubiri,
hatua zinapaswa kuchukuliwa kwa haraka, thabiti na mwitikio uwe ni kwa wadau
wote, binafsi na umma ili kuhimiza mabadiliko ya kitabia kwa ajili ya
kukabiliana na matishio hayo yanayotokana na shughuli za kibinadamu.
Kibiku ni miongoni mwa maeneo
matano ya hifadhi ambayo kwa sasa Jeshi la ulinzi la Kenya limeazimia
kuyarejesha.
Kwa mujibu wa wizara ya
Mazingira, kwa sasa misitu inafunika eneo la ukubwa wa asilimia 6.2 na serikali
imeongeza juhudi ili kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la asilimia 10 katika
siku za badaye.
Post a Comment