Dk. Shein: 'Wanyimeni Fomu za Kugombea Uongozi Wabunge, Wawakilishi walioshindwa Kutekeleza Ilani ya CCM
MAKAMU
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) Zanzibar, Dk. Ali Mohamed
Shein ameitaka Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja kutowapatia fomu
za kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu ujao Wabunge,
Wawakilishi na madiwani wanaoshindwa kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka
2015/2020.
Pia
Dk. Shein amesema suala la viongozi hao kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya CCM sio
jambo la hiari bali ni lazima kwa kiongozi yeyote aliyepewa ridhaa ya
kuwatumikia wananchi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Agizo
hilo amelitoa katika mwendelezo wa ziara zake wakati akizungumza na mabalozi wa
CCM Wilaya ya Kaskazini 'A' Unguja, huko katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Kaskazini
Unguja-Mahonda.
Dk.Shein
alisema kiongozi yeyote ndani ya CCM anayeshindwa kutekeleza kwa wakati ahadi
alizotoa kwa wananchi asipewe nafasi nyingine ya kugombea nafasi hiyo katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Aliwambia
mabalozi hao kwamba CCM haitowaonea huruma Wabunge, Wawakilishi na Madiwani
waokwepa kutekeleza majukumu yao na badala yake kukiletea Chama mzigo mkubwa
katika chaguzi mbali mbali za dola.
"Wakumbusheni
Wabunge, Wawakilishi na madiwani kutekeleza ahadi zao kwa wakati na wakikataa
basi katika uchaguzi mkuu ujao msiwape fomu za kugombea tena.",
alisisitiza Dk. Shein.
Agizo
hilo Dk.Shein alilitoa kufuatia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Idd
Ali Ame kusema kuwa Kamati ya siasa ya Mkoa wake tayari imefanya ziara ya
kuimarisha Chama katika majimbo tisa(9) ya mkoa huo na kupokea malalamiko ya
baadhi ya viongozi hao wa majimbo kushindwa kutekeleza ahadi walizoahidi kwa
wananchi.
Akizungumza
katika Mkutano huo Dk.Shein alisema Chama Cha Mapinduzi kinawategemea na
kuwaamini mabalozi katika kulinda, kutetea na kukiletea ushindi Chama kwa kila
uchaguzi kwani wao ndio waliokuwa karibu zaidi na wananchi wa makundi yote.
Amewataka
mabalozi hao kulinda maadili, miongozo na miiko ya Chama Cha Mapinduzi ili
taasisi hiyo ya kisiasa iendelee kubaki katika misingi yake ya kiuongozi na
ustawi wa demokrasia.
Pamoja
na hayo hayo Dk. Shein alisema hafurahishwi na kuripotiwa kwa vitendo vya
udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto, hivyo mamlaka husika
zinatakiwa kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaofanya matukio hayo.
Aliwakumbusha
mabalozi hao kuwa mstari wa mbele kutangaza mambo mema yanayotekelezwa na
serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili wananchi waliopo katika maeneo yao waweze
kuyafahamu.
Dk.Shein
alisema serikali inaendelea na jitihada za kutekeleza miradi ya kimaendeleo kwa
wananchi, ikiwemo ujenzi wa barabara za kisasa ndani ya Mkoa huo za maeneo ya
Mkwajuni-Kijini km 7.6.
Zingine
ni barabara za Mkwajuni-Mbuyu maji km 22, Pale-Kiongele km 4.6 pamoja na
Bububu-Kinyasini zote zikiwa ni miongoni mwa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya
mwaka 2015/2020.
Aidha
Dk.Shein alisema serikali ina dhamira ya kujenga mji wa kisasa katika eneo la
Mkokotoni ili kwenda sambamba na dhana ya kuifanya Zanzibar kuwa na miji ya
kisasa.
Nae
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdalla Juma Mabodi ameeleza kuwa viongozi
wa chama na serikali wamekuwa wakishirikiana vizuri katika kuwaletea wananchi
maendeleo.
Dk.Mabodi
amesifu juhudi za kuimarisha Chama Cha Mapinduzi zinazofanywa na uongozi mpya
wa Mkoa huo kuwa zinajenga matumaini na uaminifu kwa Wana-CCM.
Akisoma
risala ya mabalozi, Jafar Ali Haji alisema wanampongeza Dk.Shein kwa kuendelea
kuongoza serikali kwa ufanisi mkubwa, sambamba na kusimamia vizuri utekelezaji
wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa vitendo.
"Tunakupongeza
Dk.Shein kwa mambo mengi mazuri uliyoyafanya kwa maslahi ya wananchi wa Wilaya
ya Kaskazini 'A' na maeneo mengi hasa kuanzisha mfuko ya pencheni ya wazee
tunayopata shilingi 20,000 kwa kila mwezi.
Kupitia
risala hiyo walieleza kuwa tayari maagizo ya Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed
Shein, aliyotoa katika ziara zake za kiserikali mwaka jana yametekelezwa kwa
kiwango kikubwa katika vijiji vya Mbuyu tende na Mlilile na kwa sasa wananchi
wa wanapata huduma za maji safi na salama, skuli na barabara.
Mabalozi
hao walisema licha ya mafanikio hayo bado Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto
ya upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi kwa ngazi ya sekondari na msingi.
Post a Comment