Header Ads

Marzouk: Wanahabari tumieni nafasi yenu kuikomboa Jamii


WAANDISHI wa habari wametakiwa kutumia fursa waliyonayo kuwaelimisha wananchi juu ya kushiriki katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali katika maeneo yao.
 
Akizungumza na waandishi wa Habari , Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo Pemba Marzouk Khamis Sharif amesema fursa ya waandishi wa habari ni kubwa katika kuwahamasisha wananchi kushirikiana na Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo.

Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu wa saba imetekeleza miradi mingi ya maendeleo katika kisiwa cha Pemba , ikiwemo kusambaza umeme kwenye visiwa , ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na kuimarisha huduma za elimu.

Aidha Marzouk amesema ni jukumu la waandishi wa habari kuyatangaza mafanikio hayo ili wananchi waweze ,utamabua juhudi za serikali za kuwasogezea huduma za kijamii karibu yao.

Katika hatua nyengine amewataka waandishi wa habari hususani wa redio za kijamii, kutayarisha vipindi vinavyozungumzia zaidi maendeleo yaliypfikiwa , huku akiahidi kwamba Idara yake itaunga mkono kwa kushirikiana katika kuandaa vipindi hivyo.

Msaidizi Meneja Redio Jamii Micheweni Shaban Ali Abeid amesema kituo kimeandaa utaratibu wa kurusha vipindi vinavyohusua mafanikio ya serikalai ya awamu ya saba.

No comments