Uharibifu wa Miundombinu ya Barabara Kusini Pemba kikwazo kwa Wasafiri
WADAU wa
usafari Mkoa wa Kusini Pemba, wamesema kukosekana usimamizi na matumizi sahihi
wa barabara inachangia kutokea uharibifu wa miundombinu ya barabara na
kuharibika haraka.
Wamesema
kukosekana usimamizi madhubuti wa miundo mbinu ya barabara, kunachangia
uharibifu mkubwa wa barabara hizo hali ambayo pia inachangia ajali za
barabarani.
Katibu wa
Jumuiya ya Madereva Mkoa wa huo Hafidh Mbaraka Salim amesema ni vyema taasisi
husika kuchukua hatua za makusudi kudhibiti magari yenye uzito kupindukia
kupita kwenye barabara huku taasisi husika zinashindwa kuchukua hatua stahiki .
“Ukiangalia barabara
nyingi zimefanya nyufa, hii ni kukosekana kwa usimamizi wa matumizi mazuri ya
miundombinu hiyo, kwani magari yanayobeba mizigo yenye uzito mkubwa kuzitumia
bila ya kuchukuliwa hatua za kisheria” alieleza.
Katika
taarifa yake kwa ujumbe wa Bodi ya Usafiri , Hafidh ametaja sababu nyengine
ambazo zinachangia uharibu wa miundombinu hiyo kuwa ni shughuli za ujenzi kwa
baadhi ya wananchi kujenga nyumba bila ya kuzingatia utaraibu wa mipango miji.
Mkurugenzi
wa Idara ya Leseni na Usafiri Zanzibar Suleiman Kirobo amesema wameshindwa
kuchukua hatua kwa magari hayo kutokana na kukosekana kifaa cha kupimia uzito
wa gari hizo .
Kirobo
amefahamisha kuwa Idara hata gari za mchanga zimekuwa zikifanya
udanganyifu katika upakiaji wa mchanga ambaapo madereva huchukua mchanga mwingi
kuliko uwezo wa gari.
“Hata magari
yanayochukua mchanga yanachangia uharibifu wa miundombinu ya barabara,
kwani yanachukua mzigo mzito kupita uwezo wake” alifahamisha.
Mwenyekiti
wa bodi ya Usafiri Mustafa Haji Mussa amesema kuwa taasisi husika zimeshindwa
uchukua hatua za kisheria dhidi ya magari hiyo kutokana na ukosefu wa mizani ya
kupimia uzito wa kila gari yenye mzigo.
Aidha
ameeleza kuwa iwapo Serikali itamiliki kifaa hicho, mbali na kudhibiti matumizi
mabaya ya barabara, pia itasaidia kupunguza ajali za barabarani ambazo zimekuwa
zikitokea na kusababisha vifo na ulemavu wa maisha kwa baadhi ya wananchi .
“Imekuwa ni
vigumu kuweza kuyabaini na kuwatia hatiani wahusika, kwa sababu hakuna mezani ya
kupimia uzito wa magari hayo” alifahamisha .
Mkuu wa
kitengo cha usalama wa barabara wa jeshi la Polisi Zanzibar Robert Patriki
Hossein amewataka madereva na wananchi kufuata sheria za usalama barabara bila
ya kushurtishwa ili kuzuia ajali za barabarani.
Post a Comment