DC WETE aagiza Madiwani Kushirikiana na Watendaji wa Baraza la Mji Kuharakisha Maendeleo kwa Wananchi
MKUU wa
Wilaya ya Wete Abeid Juma Ali amewataka Madiwani wa
baraza la Mji Wete kushirikiana na watendaji wa baraza hilo katika
kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Akizungumza
na Madiwani wa baraza hilo katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Mji
Wete amewataka kudhibiti uvujaji wa mapato ili kuongeza ufanisi wa kazi.
Mkuu
huyo wa Wilaya amewataka madiwani hao kusimamia vyema kudhibiti ukusanyaji wa
mapato na wanatoa taarifa sahihi juu ya ukusanyaji huo.
Aidha
amewasisitiza watendaji wa baraza kufanya kazi kwa uwadilifu kwani
serekali inategemea zaidi mapato yanayokusanywa kwa ajili ya
kufanyia shughuli mbalimbali za kimaendeleo katika wananchi wake.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa baraza hilo Asaa Juma Ali
amewasisitiza madiwani kuchukua juhudi za maksudi ili kuhakikisha mapato
yanaongezeka .
Nae
Kaimu Mkurugenzi wa Baraza Hilo Salma Abuu Hamad amesema ataendelea
kushirikiana na Madiwani hao katika kutekeleza majukumu yao ili kuona
maendeleo mazuri yanapaatikana katika baraza .
Hivyo
amewataka wananchi kuondosha dhana potofu kwa watendaji wanaopita
kukusanya mapato kwani pesa hizo zinazokusanywa zinatumika katika
shughuli mbali mbali za kimaendeleo katika wilaya hiyo.
Post a Comment