Maamuzi ya Bodi ya Ligi, YONDANI ASIMAMISHWA KUITUMIKIA YANGA, HAJI MANARA apewa Onyo,
BODI
ya Ligi Tanzania, imetangaza kumsimamisha beki wa Yanga, Kelvin Yondani
kutokana na kuonekana katika video akimtemea mate beki, Asante Kwasi.
Mtendani wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amezungumza hivi punde na kusema suala lake limepelekwa Kamati ya nidhamu baada ya kuonekana haliwezi kusikilizwa na Kamati ya Saa 72 iliyokaa.
"Kwa hiyo sasa tunamsimamisha hadi hapo kamati itakapokaa na kuamua kuhusiana na suala lake," alisema Wambura.
Katika picha ya video ilimuonyesha Yondani akimtemea Kwasi raia wa Ghana katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani wa jadi, Yanga na Simba ambao walishinda kwa bao 1-0.
Suala hilo lilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau, wakiwemo waliomtetea Yondani na walioona haikuwa sahihi.

Simba
imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya watani wake Yanga mwishoni
mwa wiki.
Furaha hiyo ilimfanya msemaji wao kuingia uwanjani kumalizia shangwe na mashabiki wao.
Lakini Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa) katika kikao chake cha Mei Mosi, 2018 chini ya Mwenyekiti wake, Clement Sanga ilipitia matukio mbalimbali ya Ligi Kuu ya Vodacom, na malalamiko ya klabu za Yanga na Arusha FC na kuyafanyia uamuzi.

HAJI
MANARA
Mkuu wa
Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara amepewa Onyo Kali kwa
kuingia uwanjani kushangilia ushindi wa timu yake baada ya mchezo kumalizika.
Kitendo
chake ni ukiukwaji wa Kanuni ya 14 (11) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo,
na adhabu dhidi yake imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu
kuhusu Taratibu za Mchezo.
MBEYA
CITY
Kamati ya
Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi (Kamati ya Saa) katika kikao chake cha Mei 1,
2018 chini ya Mwenyekiti wake Bw. Clement Sanga ilipitia matukio mbalimbali ya
Ligi Kuu ya Vodacom, na malalamiko ya klabu za Yanga na Arusha FC na kuyafanyia
uamuzi.
Mechi
namba 199 (Mbeya City 1 vs Yanga 1). Klabu ya Mbeya City imepigwa faini ya sh.
500,000 (laki tano) kutokana na vurugu za washabiki wake ikiwemo kurusha mawe
na chupa uwanjani katika mechi hiyo iliyofanyika Aprili 22, 2018 kwenye Uwanja
wa Sokoine jijini Mbeya. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1)
ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Post a Comment