Waziri Mwakyembe: Wanahabari Tengenezeni Jukwaa Moja lenye Kuaminika
Waziri Mwakyembe amesema ni
vyema kujenga maslah kwa pande zote ili kuondokana na mashaka ambayo Wanahabari
na serikali wanawekeana.
Awali
Mwenyekiti wa MISA Tanzania ambao ndio waratibu wakuu wa Maadhimisho ya
Uhuru wa Vyombo vya habari Bi. Salome
Kitomari amesema kumekuwa na ongezeko la matukio ya kutekwa na kuteswa kwa
wanahabari ikiwemo la kupotea kwa mwandishi wa Gazeti la Mwananchi
Azory Gwanda aliyetoweka mnamo mwezi Novemba mwaka jana.
Bi Kitomari ameitaka Serikali kupitia
jeshi la Polisi liwatafute na kuwachukulia hatua waliotenda tukio hilo.
Aidha Kaimu Mwenyekiti kutoka jukwaa
la wahariri Tanzania Deodatus Balile amesema Uhuru wa Habari Tanzania
umebainika kuzorota huku mazingira ya wanahabari kuwa ya hofu kutokana na
kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji ikiwemo kunyang’anywa vitendea kazi.
Kwa upande wake makamu wa Rais
wa Klabu za waandishi wa habari nchini Tanzania UTPC Bi. Jane Mihanje
ameiomba Serikali kupanua wigo wa uhuru wa vyombo vya Habari na kuwalinda
kutokana na kuwa waoga kwa matukio yanayoendela juu ya Waandishi wa Habari.
Post a Comment