Uzalishaji wa Karafuu Zanzibar kwa Mwaka 2017/18 Warejesha Matumaini
JUMLA ya
tani 8,533 za Karafuu zenye thamani ya shilingi bilioni 119 zimenunuliwa na
Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) katika msimu wa vuno la zao hilo msimu
wa 2017_2018.
Mkurugenzi
fedha wa shirika hilo, Ismail Omar Bai amesema kuwa kiwango hicho kimevuka
lengo la Shirika la kununua SKrafuu tani 6,770 ambazo ZSTC ilipanga kununua kwa
msimu huu.
Bai
aliyasema hayo wakati akitoa tathimini ya utekelezaji wa kazi kwa msimu wa vuno
la karafuu kwa mwaka 2017-2018 katika mkutano wa wakulima wa karafuu wa Wilaya
ya MIcheweni uliofanyika kwenye ukumbi wa skuli ya Sekondari Micheweni.
Amesema
shirika limefanikiwa kuvuka lengo la ununuzi wa karafuu baada ya wananchi kutoa
ushirikiano na kusimamia kuuza karafuu zao kwenye vituo vya ZSTC ambavyo ndiyo
vilivyo na jukumu la kununua karafuu kutoka kwa wananchi.
"Shirika
limevuka lengo kwa msimu huu, hii imetokana na wananchi kuelimika na hivyo
kuuza karafuu kwenye vituo vya shirika la ZSTC, hivyo na tunawaomba waendelee
kutuunga mkono "alifahamisha Afisa huyo.
Mapema
akifungua mkutano huo MKuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba ambae pia ndie aliyekuwa
mgeni rasmi katika mkutano huo, Mhe. Omar Khamis Othman amesema mafanikio hayo
yametokana na wananchi kujiepusha na vitendo vya uuzaji wa karafuu kwa njia ya
magendo.
Ameema kamba,
serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama viemefanya kazi kubwa kuhakikisha
biashara hiyo haramu inadhibitiwa na wananchi kutambua umuhimu wa kuuza
karafauu zao kwenye vituo vya ZSTC.
Aidha Mkuu wa mkoa amewasisitiza wakulima kuacha
tabia ya kushirikiana na wafanya biashara wa magendo ya karafuu ambao zaidi
wanajali maslahi yao binafsi hivyo kusababisha serikali kukosa mapato yake.
"Nachukua
fursa hii kulipongeza shirika kwa kufanikiwa kuvuka lengo , hii imetokana na
ushirikianao uliooneshwa na wakulima baada ya Serikali kupitia vyombo vya
ulinzi kuimarisha ulinzi na kudhihiti magendo ya karafuu," alisema.
Naye
mwanaheria wa Shirika la ZSTC Ali Hilali Vuai amewataka wananchi kufuata sheria
bila ya kushurutishwa katika kuilinda mikarafuu pamoja na zao la karafuu kwa
ijumla.
Aidha
mwanasheria amefahamisha kuwa zipo sheria ambazo zinaweza kumtia hatiani mwananchi
ambaye atakwenda kinyume na matakwa ya sheria iikiwa ni pamoja na kuhamisha
karafuu bila ya kufuata kibali kutoka serikalini sambamba na kuanika karafuu
sehemu ambazo sio sahihi.
Naye Ostadhi
Omar Hamad akitoa mada ya uadilifu katika Biashara ya karafuu amesema ni vyema
wananchi kujiepuesha na vitendo vya udanganyifu wanapokwenda kuuza karafauau zao
kwenye vituo vya ZSTC.
Amesema kuwa
tabia ya baadhi ya wakulima kuchanganya karafuu na makonyo ili kuongeza uzito ,
ni jambo ambalo linasababisha uchafu wa karafuu na hivyo kuweza kushusha ubora
wake kwenye soko la dunia.
Amesema
kitendo cha Serikali kupandisha bei ya zao la karafuu ili kuwaweza wakulima
kupambana na umaskini na hivyo kukuza kipato cha nchi na wananchi wake.
Mkutano huo
umewakutanisha maafisa kutoka Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC,
Maofisa wa Serikali Wilaya pamoja na
wakulima ukiwa na lengo la kujadili maendeleo ya Karafuu katika Wilaya ya
Micheweni, ambapo pia Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, aliweza
kukabidhi vyeti kwa Wakulima Bora wa Zao hilo kwa Mwana 2017/18.
Mgeni Rasmi, ambae pia ni Mkuu
wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe. Omar Khamis Othiman akikabidhi Kadi ya ZSTC kwa
mkulima wa Karafuu wakati wa Mkutano huo.
|
(PICHA ZOTE NA Gaspary Charles-Micheweni Redio)
Post a Comment