Waziri wa Kilimo Zanzibar aagiza watendaji Wizara hiyo kuongeza kasi kiutendaji
WAFANYAKAZI Wa Wizara Ya
Kilimo ,Maliasili, Mifugo Na Uvuvi Kisiwani Pemba Wametakiwa Kudumisha
Mshikamano Na Umoja ,Ili Waweze Kuwapatia Wananchi Huduma Bora Kwa
Wakati.
Kauli Hio Imetolewa Na Waziri Wa Wizara Hio, Mh.
Rashid Ali Juma, Katika Mkutano Wa Kujitambulisha Kwa Wafanyakazi Hao Kufuatia
Mabadiliko Ya Uongozi Uliokuwepo, Hukokatika Ukumbi Wa Kilimo Weni, Wete, Mkoa
Wa Kaskazini Pemba.
Mh.Rashid Amesema Kuwa, Asilimia Kubwa Ya Uchumi Wa
Wananchi Unatokana Na Wizara Ya Kilimo Hivyo Juhudi Za Pamoja Zinahitajika
Kuongeza Kasi ,Ili Kuona Malengo Yanafikiwa.
Akihimiza Utendaji Kazi Katibu Mkuu Wa Wizara Ya
Kilimo, Bi Maryam Abdalla Juma, Amewataka Watendaji Walio Katika Ugatuzi Kwa
Upande Wa Madaraka Kutekeleza Majukumu Yao Ipasavyo Bila Ya Wasiwasi
Pamoja Na Kueleza Matatizo Yao Pindi Wanapohitaji Kusaidiwa ,Ili Waweze
Kuiwakilisha Vyema Taasisi Yao.
Nae, Kaimu Afisa Mdhamini Wa Wizara Ya Kilimo, Sharif
Mohd Faki, Kwa Niaba Ya Wafanyakazi Wa Wizara Hio Pemba Ameahidi Huyafanyia
Kazi Maagizo Waliopewa Pamoja Na Kuuomba Uongozi Kulipatia Ufumbuzi Tatizo La
Ukosefu Wa Wafanyakazi Katika Wizara Hio.
Post a Comment