Rais Xi Jinping atoa mwito wa kujenga vyuo vikuu vya kisasa vyenye umaalum wa China
Rais Xi Jinping wa China ametoa
mwito wa kujenga vyuo vikuu vya kisasa vyenye umaalum wa China, ili kuwalea
watu kujiunga na mkondo wa ujamaa.
Rais Xi Jinping amesema hayo
alipofanya ziara ya ukaguzi katika chuo Kikuu cha Beijing, kwa ajili ya
maadhimisho ya siku ya vijana ya China na maadhimisho ya miaka 120 ya chuo
kikuu cha Beijing, ambayo yote yameangukia leo tarehe 4 Mei.
Baada ya kufahamishwa kuhusu
mafanikio ya hivi karibu ya chuo Kikuu cha Beijing kwenye mambo ya utafiti na
uhandisi, Rais Xi alikumbusha kuwa uvumbuzi ni injini kuu ya maendeleo, na
sehemu muhimu ya nguvu ya taifa na kiini cha ushindani.
Post a Comment