Rais wa Zambia azindua mpango wa kupanda Miti
Rais Edgar Lungu wa Zambia
amezindua mpango wa kuhamasisha watu kupanda miti na kuhimiza maendeleo ya
uchumi kwa kutegemea miti, ikiwa ni sehemu ya ajenda ya nchi hiyo kufanya
uchumi wake kuwa na vyanzo mbalimbali.
Viongozi wa Zambia
wanakubaliana kuwa Zambia ni moja ya nchi zilizoko kusini mwa Sahara zenye
raslimali nyingi za misitu, lakini rais Lungu ameeleza wasiwasi kuwa kuendelea
kwa ukataji miti bila udhibiti kunatishia mustakabali wa misitu ya nchi hiyo.
Amesema mpango huo unalenga
kuhimiza maendeleo ya uchumi kwa kutegemea miti ikiwa ni sehemu ya ajenda ya
nchi hiyo ya kuepukana na kutegemea shaba peke yake, na kupunguza athari mbaya
ya mabadiliko ya hali ya hewa.
Post a Comment