Taasisi za Elimu Zanzibar zatakiwa kufuatilia Historia ya Viongozi wa Kitaifa
MKUU Wa Kitengo Cha Fat-Wa Na Utafiti Kutoka Ofisi Ya
Mufti Zanzibar Sheikhthabit
Nouman Jongo Ameviomba Vyuo Na Taasisi Za Elimu Kuwa Na
Utaratibu Wa Kufuatilia Historia Za Viongozi Waliotangulia Ambao Walipigania
Kuleta Maendeleo Nchini.
Akizungumza Katika Ziara Ya Wanafunzi Wa Chuo Cha Utawala Wa
Umma Katika Sehemu Za Kihistoria Amesema Utaratibu Huo Pia Utawasaidia Kuelewa
Juhudi Zilizochukuliwa Na Viongozi Hao Ambao Walijitolewa Kupigania Uhuru Wa
Nchi Na Maendeleo Ya Jamii.
Akielezea Lengo La Ziara Hiyo Rais Wa Serikali Ya Wanafunzi Wa
Chuo Hicho Bw Suleiman Ali Abdallah Amesema Ni Kuwaenzi Waasisi Wa Nchi Pamoja
Na Kujifunza Mbinu Zilizotumiwa Katika Uongozi.
Katika Ziara Hiyo Wanafunzi Hao Wametembelea Kaburi La
Rais Wa Kwanza Wa Zanzibar,Marehemu Abeid Amani Karume, Rais Wa Awamu Ya Pili
Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi Na Marehemu Idrisa Abdul-Wakil.
Post a Comment