Balozi Seif Ali Idd awasihi wanafunzi kuyapenda Masomo ya Sayansi kwa Maendeleo ya Taifa
MAKAMO wa pili wa
Rais Mhe Balozi Seif Ali Idd amewataka wanafunzi kupenda kusoma masomo ya
sayansi ili kuifanya serikali kuacha kuagiza walimu wa masomo ya sayansi kutoka
nje ya nchi .
Amesema lengo la
serikali ni kujitosheleza kwa wataalamu , hivyo ni vyema wanafunzi kusoma kwa
juhudi na maarifa ili waweze kuyafahamu masomo yao ambayo pia yanasoko katika
uimwengu wa leo.
Akikabidhi msaada
wa madawati uliotolewa na mfanyabiashara Said Bopar kwa uongozi Wizara YA Elimu kwa ajili ya
Skuli ya Micheweni , Balozi Seif amewahimiza wanafunzi kuhakikisha wanasoma
masomo ya hisabati , Phiskia pamoja na kemia .
Aidha Balozi Seif Ali
Idd amewataka wazazi kufuatiliamaendeleo ya watoto wao skuli kwa kuhakikisha
wanahuduhuria masomo yao , jambo ambalo linawafanya wasome kwa bidii .
Wakati huo huo
Balozi Seif amekabidhi vifaa vya upasuaji katika Hospitali ya Micheweni na
kuwataka Madaktari kuvitunza na kuvitumia kama ilivyokusudiwa.
Post a Comment