RC KAS PEMBA: 'Serikali itaendelea kutumia rasilimali zake kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi '
SERIKALI
ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imesema itaendelea kutumia rasilimali zake
zinazopatikana ndani ya Mkoa ikiwemo madaktari kwa ajili ya kutoa huduma bora
za matibabu kwa wananchi .
Hayo
yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman wakati
alipotembelea Hospitali ya Micheweni ambayo inatarajia kupandishwa hadhi ya
kuwa hospitali ya Wilaya.
Amesema
pamoja na changamoto ya upungufu wa Madaktari katika Hospitali hiyo, lakini ni
vyema waliopo kufanya kazi kwa weledi, juhudi na kuagiza uongozi wa
Hospitali hiyo kuwachukulia hatua Madaktari wazembe.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa wakati Hospitali hiyo inaelekea kuwa Hospitali
ya Wilaya, Serikali ya Mkoa itahakikisha azma hiyo inafanikiwa na wananchi wa
Micheweni waendelee kunufaika na matunda ya Serikali yao ya awamu ya
saba.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Salama Mbarouk Khatib amesema maandalizi ya Hospitali
hiyo kufikia hadhi ya kuwa Hospitali ya Wilaya yanaendelea vyema ambapo baadhi
ya vifaa vya upasuaji vimeshawasili .
Daktari
Dhamana wa Hospitali hiyo Mbwana Shoka amesema tayari jengo la operesheni ya
akinamama limekamilika kwa zaidi yaaslimia tisini.
Shoka
amefamamisha kwamba baada ya kukamilika ujenzi wa jengo la upasuaji wa
akinamama , bado jengo la upasuaji wa jumla halijakamilika na kuiomba Serikali
ya Mkoa kusaidia hatua iliyofikia ili jengo hilo nalo likamilike .
Post a Comment